Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yakataa ombi la Libya la kusitisha kujisalimisha kwa Saif Al-Islam Gaddafi :

ICC yakataa ombi la Libya la kusitisha kujisalimisha kwa Saif Al-Islam Gaddafi :

Kitengo cha rufaa cha mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC Alhamisi kimekataa ombi la uongozi wa Libya la kutaka kumsalimisha kwa mahakama hiyo Saif Al-Islam Gaddaffi na kukumbusha kwamba Libya ina wajibu wa kumsalimisha bwana Gadaffi kwenye mahakama hiyo.

Serikali ya Libya iliwasilisha ombi Juni 7 mwaka huu ikitaka kusitishwa kumsalimisha mshukiwa wakati uamuzi wa mahakama ukisubiriwa dhidi ya Libya kupinga kesi dhidi ya mshutumiwa Gadaffi.

Kitengo cha rufaa hakikuridhika na sababu zilizotolewa na Libya za kwa nini kumsalimisha bwana Gadaffi kwenye mahakama hiyo kutazusha hali ya taharuki au hali ambayo itakuwa vigumu kuirekebisha.

Hali ya Libiya ilifikishwa katika mahakama ya ICC na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa azimio namba 1970 mnamo tarehe 26 Februari 2011 na tarehe 27 Juni 2011 mahakama ya ICC ikatoa kibali cha kukamatwa kwa Muammar Mohammed Abu Minyar Gaddafi, Saif Al-Islam Gaddafi na Abdullah Al-Senussi kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu yanayodaiwa kufanyika Libya kuanzia Februari 15 hadi Feberuari 18 mwaka 2011 kwa kutumia vyombo vya serikali na majeshi ya usalama.