Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ashutumu dhuluma zinazoendeshwa na jeshi la DRC dhidi ya wanamgambo wa M23

Ban ashutumu dhuluma zinazoendeshwa na jeshi la DRC dhidi ya wanamgambo wa M23

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesikitishwa na ripoti kuhusu kudhulumiwa kwa wafungwa wa kundi la M23 na pia ripoti za kuchomwa kwa miili ya wanangambo hao vitendo vinavyondeshwa na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO umelitilia maanani zaidi suala hili ukilitaka jeshi la DRC kuchunguza madai hayo na kuwafikishia wahusika mbele ya sheria. Kwa upande wake Ban ametaka serikali ya DRC kuwafikisha mbele ya sheria na kuvichukuliwa vitendo hivyo kuwa ukiukaji wa haki za binadamu na sheria ya kimataifa. Amezitaka pande husika kujiepusha na vitendo kama hivyo na kutafuta njia za kusuluhisha mzozo ulio nchini DRC kwa amani.

(SAUTI YA CRUZ)