Tusiruhusu dini kutumiwa kueneza chuki na migawanyo: UNAOC

17 Julai 2013

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mwakilishi Mkuu wa Muungano wa Ustaarabu katika Umoja wa Mataifa, UNAOC, Nassir Abdul Aziz Al-Nasser, ametoa wito dini zilindwe kutokana na watekaji wanaotaka kuzitumia kwa faida zao binafsi. Bwana Al-Nasser ameyasema hayo wakati wa mkutano wa marafiki wa Muungano wa Ustaarabu ya Umoja wa Mataifa leo mjini New York, akiongeza kuwa wanadamu wote wana maadili mengi ambayo yanafanana, licha ya kuwa imani tofauti za kidini.

Amesema wanachama wa Umoja wa Mataifa wamerithia kanuni katika mkataba wake mkuu, ambazo kila mmoja anapaswa kuendeleza bila kuchoka, katika juhudi za kujenga amani na kuendeleza kuvumiliana, ambayo ndiyo malengo makuu ya jumuiya ya ustaarabu.

Bwana Al-Nasser amesema inasikitisha kuwa kanuni hizi zinatishiwa na watu wenye misimamo mikali ambao wanaendelea kutumia vibaya ujumbe wa amani wa dini ya Kiislamu na imani zingine, huku akirejelea ujumbe wa mtoto wa Kipakistani Malala Yousafzai kwenye Umoja wa Mataifa mnamo Julai 12, wa umuhimu wa kuwapinga wale wanaotumia dini kwa malengo yao potofu.

Ujumbe wa Bwana Al-Nasser umesisitizwa na Naibu Katibu Mkuu, Jan Eliasson, ambaye pia akimnukuu Malala, amesema Muungano wa Ustaarabu uliundwa ili kukabiliana na migawanyo na chuki, kwa kutoa nafasi ya mazungumzo na maridhiano. Amesema dini zote zinatakiwa zikubali maadili yetu ya pamoja na ubinadamu.

Ameongeza kwamba viongozi wa kidini wana ushawishi mkubwa kwa wafauasi wao, na ikiwa watahubiri chuki na kutovumiliana, wanapanda migawanyo, mizozo na ghasia, lakini wakihubiri ujumbe wa kuelewana na undugu, wanaweka msingi wa kuaminiana, kuelewana na amani na usalama wa kudumu.