Haturudi nyuma licha ya askari kuuliwa: UNAMID
Siku chache baada ya kuuwawa kwa askari saba walinda amani wa Umoja wa Mataifa Darfur Sudan, Kamanda Mkuu wa kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa Darfur UNAMID, Luteni General Wynnjones Kisamba amesema askari waliosalia katika jukumu hilo wako tayari kuendelea na kazi ya kulinda amani licha ya changamoto za mashambulizi kama hayo.
Katika mahojiano maalum na ishaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa kutoka katika jimbo hilo, General Kisamba amesema amaezungumza na askari hao kuwatia shime kusonga mbele.
(SAUTI KISAMBA)
Askari saba kutoka kikosi cha Tanzania huko Darfur waliuwawa na watu wenye silaha ambao hawajajulikana