Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa dola milioni 172 kwa ajili misaada ya dharura katika maeneo yalopuuzwa

UM watoa dola milioni 172 kwa ajili misaada ya dharura katika maeneo yalopuuzwa

Mratibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, ametangaza leo kutolewa kwa dola milioni 72 kwa huduma za kibinadamu katika jumla ya nchi 12 duniani zenye mizozo ilopuuzwa. Kiwango hiki kipya cha fedha kinafanya jumla ya fedha zilizotengwa na mfuko wa CERF kwa ajili ya huduma za dharura katika maeneo yenye uhaba wa ufadhili mwaka huu kufika dola milioni 172, ambacho ndicho kiasi kikubwa zaidi kuwahi kutolewa katika mwaka mmoja pekee.

Fedha hizo zitasaidia kufadhili huduma za kibinadamu katika nchi za Bangladesh, Chad, Colombia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa Korea, Haiti, Madagascar, Mauritania, Myanmar, Niger, Pakistan, Ufilipino na Somalia, ambayo itapokea dola milioni 20.