Wakimbizi wa DRC wana wakati mgumu:UNHCR

16 Julai 2013

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanaonya juu ya hali mbaya ya kibinadamu Magharibi mwa Uganda ambapo juhudi za kuwafidhi sehemu salama maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , DRC wakati huu ambapoa juhudi za kuwahifadhi sehemu salama wakimbizi hao zinafanywa.Taarifa zaidi na George Njogopa(TAARIFA YA GEORGE)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema kuwa kiasi cha wakimbizi 70,000 wametawanyika katika maeneo ya mlimani na kujikuta wakiwa kwenye hali ngumu kutokana na mazingira ya eneohilo.

Lakini UNHCR inasema kuwa hadi sasa jumla ya wakimbizi 2,000 tu ndiyo waliosafirishwa hadi kwenye vituo kimoja kilichopo umbali wa kilometa 20 kutoka mpaka waUgandana Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC.

Wafungwa wengi wanasema kuwa wangependelea kuendelea kusalia kwenye maeneo hayo ya mpakani kwani wanadai kuwa kwao ni rahisi kurejea tena nyumbani.

Makundi mengi ya wakimbizi yanasambaa kwenye eneohilo la mpaka, lililoko kaskazini wa mpaka naUganda, tangu kulipuzuka machafuko hayo hapo siku ya alhamisi katika mji wa Kamango uliopo mashariki mwa DRC. Adrian Edwards ni msemaji wa  UNHCR .

“Katika wakati mmoja, pamoja na kwamba serikali ya Congo inawahamasisha watu wake kurejea nyumbani, lakini wakimbizi hawa hawako tayari  kurejea nyumbani mara moja kutokana na hali ya sintofahamu inayoendelea katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.Tunawasiwasi kutokana na hali ilivyo wakati huu.Wakimbizi wameendelea kutawanyika katika maeneo ya milimani kwenye eneo la mpaka,ni ngumu sana kwao kupata maji ya kunywa na chakula, mazingira ya kiafya pamona na usafi jumla ni tatizo kubwa. Tunaamini kwamba kadri wanavyoendelea kuishi kwenye eneo hilo la mpakani ndivyo kunavyozidi kujitokeza hatari za kuzuka magonjwa ya mlipuko.