Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasudan Kusini waliokwama mpakani wawasili Juba:IOM

Wasudan Kusini waliokwama mpakani wawasili Juba:IOM

Raia wa Sudan 978 waliokuwa wakirejea nyumbani na kukwama kwenye mji wa Renk mpakani wamewalisi Juba Jumanne kwa msafara ulioandaliwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.Tishali nne zilizobeba watu hao na mizigo yao ziliondoka Rwnk Renk jimbo la Upper Nile tarehe 30 Juni wametumia wiki mbili hadi kuwasili Juba wakipumzika katika miji ya Melut, Malakal, Shambe na Bor ambako watu wengine walishuka ili kuelekea sehemu zingine.