Mkurugenzi mkuu wa UNESCO ataka kuchukuliwa hatua za kulindwa maeneo ya kitamaduni nchini Syria

16 Julai 2013

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la elimu ,sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ameelezea mshangao wake kutokana na ripoti za kuharibiwa kwa maeneo zaidi ya kitamaduni nchini Syriabaada ya vyombo vya habari kuripoti uharibufu kwenye eneo la kitamaduni la Crac des Chevaliers.

Maeneo hayo ni mfano wa mijengo iliyojengwa kati ya karne ya 11 na 13. Bokova ametaka wahusika wote kusitisha uharibifu huo  na kuzitaka pande zote kuchukua hatua kuhakikisha kuwa maeneo hayo yamelindwa. Wakati wa kikao cha kamati inayohusika na utamaduni duniani kilichoandaliwa nchini Cambodia maeneo sita ya kitamaduni nchini Syria yaliorodeshwa kama maeneo ya kitamaduni yaliyo kwenye hatari .

Wanachama wote wa kamati inayohusika na utamaduni duniani wamezitaka pande zote kujiepusha na vitendo ambavyo vitasasababisha uharibifu zaidi kwa maneo ya kitamaduni nchiniSyriana kuheshimu sheria za kimataifa zinazohitaji kulindwa kwa maeneokamahayo. Bokova amesema kuwa UNESCO iko tayari kushirikiana na pande zote katika jitihada za kulinda maeneo hayo ikiwa hali ya usalama itaruhusu.