Wataalamu wa haki za kibinadamu wa UM wamekaribisha msamaha wa kifalme, Cambodia

15 Julai 2013

Mratibu  Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Ripoti juu ya hali ya haki za binadamu  Cambodia, Surya P. Subedi, amekaribisha leo  kupewa msamaha wa kifalme kiongozi wa upinzani Sam Rainsy, wa Cambodia  kabla ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 28 Julai 2013.

Sam Rainsy,ambaye ni kiongozi wa chama cha ukoaji  wa Cambodia alitiwa hatiana January 2010 kwa makosa ya uharibifu wa mali na kuchochea ubaguzi wa rangi. Alihukumiwa kifungu cha miaka miwili kwa kosa la kwanza, na kifungu cha miaka 10 kwa kosa la pili.Hata hivyo hukumu hiyo ilisomwa bila yeye kuwepo mahakani na tangu wakati huo ameendelea kuishi uhamishoni.

Akizungumzia hatua ya kufunguliwa njia kwa kiongozi huyo, mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa anaamini sasa serikali itachukua mkondo sahihi ili kumwezesha Rainsy kushiriki kikamilifu katika siasa za taifa lake