Lowassa achambua Malengo ya Milenia.

15 Julai 2013

Shirika la Un foundation wiki iliyopita liliandaa mkutano uliojadili tathmini ya utekelezaji wa maendeleo ya milenia pamoja na nini kifanyike baada ya ukomo wake mwaka 2015. Hoja iliyogubika mkutano huo ilikuwa nafasi ya wazee katika malengo hayo yanayoelekea ukingoni na mapendekezo kuhusu mkakati wa maendeleo baada ya 2015.

Miongoni mwa walioalikwa kushiriki mjadala huo ni Wazri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa ambaye amekutana na mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa na kufanya mahiojiano naye hapa mjini New York.

Bwana Lowasa anaanza kwa kuelezea dhima ya mkutano pamoja na kuleza utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia hususani kwa nchi zinazoendelea.