Ban aishukuru Ufaransa kwa mchango wake katika kulinda amani

15 Julai 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameishukuru serikali ya Ufaransa kwa mchango wake muhimu na kwa kujitolea kwake ili kuleta amani, usalama, maendeleo kwa watu waMali. Joshua Mmali na maelezo Zaidi.(RIPOTI YA JOSHUA MMALI)

Ban ambaye leo amehitimisha ziara yake nchini Ufaransa ameyasema hayo alipokutana na Rais wa nchi hiyo bwana Hollande

 (CLIP YA BAN )

 

Bila mchango huo muhimu wa Ufaransa na pia bila  uamuzi wa Rais Hollande, watu waMali hawangeweza kuwa na utulivu, uhuru na usalama wakati huu.Asante tena. Nina matumaini kaika uongozi wako na kuendelea kwa msaada wako. Kama unavyojua, ujumbe wa MINUSMA unakosa vifaa kadhaakama vile helikopta za kijeshi zilizo na silaha.”

Jana alasiri, Ban pia alikutana na Rais Traoré wa Mali. Akamwambia kuwa uchaguzi wa urais lazima ufanyike katika mazingira yenye utulivu, bila vurugu, kwa njia inyaminika na kwa amani. Na matokeo ya uchaguzi wa urais lazima yaheshimiwe na vyama vyote. Amemshauri kuunda tume ya maridhiano na mazungumzo baada ya uchaguzi kwa ajili ya utulivu wa kudumu.Mbali ya Mali wamelikugia sula la mzozo unaoendelea nchini Misri

(BAN MISRI CLIP)

“Kuhusu Misri, nataka kusisitiza kwamba ni muhimu kujizuia kabisa na kwamba hali ya baadaye ya nchi lazima ijadiliwe kwa amani. Ni kweli tuko katika wakati muhimu.Ni muhimu kwamba Wamisri wote wafanye kazi kwa pamoja kwa ajili ya kurejea kwa amani na utaratibu wa kikatiba na utawala wa kidemokrasia.”

 

Amesema viongozi wa kisiasa nchini Misri wana wajibu wa kuonyesha, kwa maneno yao na kwa vitendo vyao, dhamira yao ya  kuwa na mazungumzo ya amani na ya kidemokrasia wakishiirikisha wadau wote wa Misri.