ILO na Uingereza kuwalinda wasichana na wanawake dhidi ya utumwa

15 Julai 2013

Mradi mpya wa kusaidia kuwalinda wasichana na wanawake takribani 100,000 dhidi ya mfumo mbaya kabisa wa usafirishaji haramu wa watu kwa ajili ya kufanya kazi zisizostahili baraniasiaumezinduliwa hii leo.Mradi huo utaendeshjwa na kitengo cha maendeleo ya kimataifa cha serikali ya Uingereza na shirika la kazi duniani ILO.

Serikali ya Uingereza inawekeza pauni milioni 9.75 katika kipindi cha miaka miatano katika mradi huo ili kukabiliana na tatizo linalojulikanala njia za kusafirisha wafanyakazi baina ya nchi za Asia Kusini kama vileBangladeshnaNepalhadi Mashariki ya Kati zikiwemo nchi zaJordan, Falme za nchi za Kiarabu (Emarati) na Lebanon.

Karibu watu milioni 21 wanasafirishwa kiharamu na kushinikizwa kufanya kazi kote duniani, huku wengi wao wakitoka baraniasiana wanawake na wasichana ndio waathirika wakubwa zaidi.