Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya kutoa misaada yaongeza huduma zake eneo la Pibor

Mashirika ya kutoa misaada yaongeza huduma zake eneo la Pibor

Wakati hayo yakijiri makundi ya vijana waliojihami wamekabiliana  kwenye maeneo tofauti ya nchi . Zaidi ya majeruhi 200 kwenye makabiliano hayo wamesafirishwa  kupewa matibabu na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS. Umoja wa Mataifa kupitia huduma zake za anga pamoja na shirika la afya duniani WHO wanakagua eneo la Menyapol ili kuweza kuwasafirisha wale waliojeruhiwa  zaidi kwenda Bor ambapo watapewa matibabu.