Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ging awavulia kofia wafanyikazi wa misaada ya kibinadamu

Ging awavulia kofia wafanyikazi wa misaada ya kibinadamu

Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Misaada katika Umoja wa Mataifa, OCHA John Ging, amewapa heshima wafanyikazi wa misaada ya kibinadamu Somalia na kutoa wito wa uwekezaji mkubwa ili kuvunja mzunguko wa migogoro nchini humo, mwishoni mwa ziara ya siku mbili Mogadishu na Nairobi Ijumaa.

Ging ameelani mashambulizi yalopelekea kupoteza kwa maisha katika kituo cha Umoja wa Mataifa Juni 19 mwaka huu, akiongeza kuwa moyo wake unawaendea jamii na marafiki ya wale wote waliopoteza maisha yao kwa ujasiri wao katika kuwalinda wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Akmeongeza kuwa ushujaa wao ni dhahibu na hautasahaulika.

Bwana Ging alikutana na viongozi wa Serikali ya Somalia, Umoja wa Mataifa , AMISOM, washirika wa kibinadamu na jumuiya ya wafadhili wakati wa ziara yake. Alitoa wito kwa wale wote walio na ushawishi kuimarisha jitihada zao maradufu kwa kutoa mazingira salama ya kazi kwa wafanyikzi wa kibinadamu huku akionyesha heshima yake na shukrani kwa ajili ya kuendelea kujitolea kwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu nchini Somalia kufikia wote wale wenye mahitaji, licha ya hatari iliyopo.

Licha ya kuimarika kwa hali ya kibinadamu nchini Somalia, mahitaji bado ni mengi. Takriban watu milioni 1 wanahitaji misaada ya kibinadamu haraka na zaidi ya milioni 1.7 wanahitaji msaada endelevu kuepuka kusalia katika mgogoro. Mmoja kati ya watoto saba nchini Somalia wana utapiamlo na hivi karibuni ugonjwa wa polio umeshuhudiwa baada ya zaidi ya miaka sita bila kesi yoyote kuripotiwa. Lakini kwa ombi zima la rufaa ya Somalia la kibinadamu kwa ajili ya 2013, ni asilimia 33 tu imefadhiliwa.