Kwenye Siku ya Malala Duniani vijana waunga kampeni ya Elimu Kwanza

12 Julai 2013

Katika kuadhimisha Siku ya Malala Duniani kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 12 Julai, vijana mia moja kutoka kote duniani wamekusanyika kwenye Umoja wa Mataifa na kulitwaa jukwaa la ukumbi wa Baraza la Usalama. Vijana hao, ambao wameshuhudia na kumsikiliza mtoto Malala akilihutubia Baraza la Usalama, wamebadilishana pia mawazo kuhusu jinsi ya kuliendesha gurudumu la mkakati wa kimataifa wa Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon wa Elimu Kwanza.

Mmoja wa vijana hao ni Lian Kariuki kutoka Kenya, ambaye ni mwanafunzi kwenye chuo cha Green Mountain College hapa Marekani. Amezungumza na Joshua Mmali na kwanza kumwelezea anavyofahamu umuhimu wa siku hii ya Malala.