Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ya watoto wa kike yapigiwa debe!

Elimu ya watoto wa kike yapigiwa debe!

Watoto wa kike wamekuwa wakinyimwa fursa za elimu sehemu mbalimbali duniani kutokana na sababu nyingi mojawapo ikiwa ni utamaduni na umaskini .

Katika makala hii Joseph Msami anamulika tatizo hilo wakati huu ambapo mtoto mwanaharakati wa elimu Malala Yousfzai ambaye alipigwa risasi mwaka jana na wanamgambo wa Taliban kutokana na msimamo wake wa kutetea bayana elimu, ameadhimisha miaka kumi na sita na kupewa heshima ya kila July 12 kuwa siku ya Malala duniani.