Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angelique Kidjo ampa ujumbe mzito Malala

Angelique Kidjo ampa ujumbe mzito Malala

Mwanamuziki mashuhuri na mwanaharati wa haki za wanawake Angelique Kidjo amekutana na mtoto mwanaharakti Malala Yousfzai ambaye ameadhimisha miaka kumi na sita leo na kumtaka kuendeleza harakati zake katika kufikia dunia katika swala la elimu kwa watoto wa kike.

Akongea muda mfupi baada ya kuhudhuria hafla maalua makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ambapo Malala aliyepigwa risasi mwaka jana na wanamgambo wa Taliban kutokana na msimamo wake wa kutetea bayana elimu, alihutubia leo, Kidjo ambaye ni balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wa toto UNICEF, amesema amezungumza naye baada ya hotuba yake na kumwalika Afrika.

(SAUTI KIDJO)

Kitu ambacho nimemwambia ni kwamba aendelee kuwa kiongozi katika neoe hili la wanawake duniani kote lakini jambo tunalohitaji kuwa nalo makini ni kuwaelimisha wavulana sawa na wasichana, ili vita hii itokomee lazima tuwe na wanaume wanaowaruhu wanawake waje pamoja nasi katika ulingo tupabmane pamoja na kuongeea na wanaume wengine. Na nikamwabia aje Afrika kadhalika aongee na wasichana ili waone hawako peke yao katika tatizo hili.

Mwanamuziki huyo ambaye ni mzaliwa wa Benin amemuhakikishia Malala ushirikiano muda wowote katika kutimiza malengo yake.