Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yajipanga kuwafikia wenye virusi vya ukimwi duniani

UNAIDS yajipanga kuwafikia wenye virusi vya ukimwi duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Ukimwi , UNAIDS, limezindua mkakati mpya wa kuwafikiwa watu milioni kumi na tano duniani wanaotumia dawa za kurefusha maisha baada ya ifikapo mwaka 2015.

Lengo hilo ambalo liliwekwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2011 lilikusudia kuzipa nchi na washirika njia za vitendo na nadharia katika kuwafikia walengwa ambapo waathirika wanaweza kuishi maisha marefu zaidi na kwa afya.

Kwa mujibu wa UNAIDS upimaji wa umma na ushauri nasaha ni njia muafaka ya kusaidia kutokomeza ugonjwa huo hasa ikizingatiwa kwamba waathirika huanza kutumia dawa za kurefusha maisha baada ya kugundua wana maambukizi. Upimaji huo umeonekana kuwa na mafanikio katika baadhi ya nchi ikiwemo Kenya, Malawi, Uganda Tanzania Zambia na Afrika ya Kusini.

Akitoa wito katika kutekeleza mkakati huu, Mkurugenzi Mtendaji wa mkfuko wa kimataifa wa kupamana na Ukimwi, kifua kikuu na malaria Mark Dybul amesema ni lazima kufanya kazi kwa bidii kuushinda ukimwi ambao ni tishio katika afya ya jamii na kuongeza kuwa juhudi za pamoja zinahitajika kutoka kwa wadau wote.