UNHCR yasema kuwa hali imeboreka kwenye kituo cha wahamiaji katika kisiwa cha Manus

12 Julai 2013

Shirika la kuhudmia wakimbizi la Umoja wa Mataiafa UNHCR limetoa ripoti yake ya pili kuhusu kituo kilicho kwenye kisiwa cha Manus nchini papua New Guinea ambacho kwa sasa kinawahifadhi watafuta hifadhi 250 waliopelekwa huko na Australia kuandikishwa. Jason Nyakundi anaripoti.

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Ripoti hiyo inatokana na matekeo ya kundi moja la Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR lililikitembelea kisiwa cha Manus kunzia tarehe 11-13 mwezi Juni. Ziara hiyo ilikuwa ni ya kukagua hali kwenye kituo waliko wahamiaji kuambatana na makubalino ya mwaka 1951. Kundi hilo lilikutana na watafuta hifadhi , maafisa kutoka kwa serikali ya Papua New Guinea na Australia na wafanyikazi kutoka kwa mashirika yanayotoa huduma. Edrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

Ujumbe huo ulipata kuwa hali imeboreka kinyume na ilivyokuwa mwezi Januari wakati wa ziara yake ya mwisho lakini hata hivyo viwango vilivyopo hafijaafikia vile vya kimataifa.