Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kwa watoto wa kike ni haki sio hiari:Brown

Elimu kwa watoto wa kike ni haki sio hiari:Brown

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika elimu kimataifa Gordon Brown amesema ni muhimu serikali na wale wenye misimamo mikali wakatambua na kutekeleza elimu kwa watoto wa kike kama haki ya msingi nasio kitu cha hiari.

Akiongea mjini New York muda mchache kabla ya maadhimishio ya miaka 16 ya mtoto Malala Yousfzai ambaye alijeruhiwa kwa risasi na watalibani huko Pakistani mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na msimamo wake wa kutetea bayana elimu kwa mtoto wa kike, Brwon amesema mitizamo ya wengi umebadilika nchini Pakistan na ni jukumu la Umoja wa Mataifa kuwawezesha kuzungumza kwa hadharani kutoa rasilimali na huduma bora za elimu.

(SAUTI BROWN)

Elimu kwa watoto wa kike ilikusudiwa kuwa haki na sio ya kunyimwa,ni namna giin tunavyoweza kuwawezesha kuongea na sio kuwa kimya,tumeona mwaka 2000 shule ziichomwa nchini Pakistan na Afghanistan tumeona walimu wakiuwawa kwa kuwa wamewafundisha wasichana na pia wasichana wakishambuliwa na kuteswa kutokana na utayari wao wa kwenda shule,lakini nimeona nilivyokwenda Pakistan mara ya mwisho mabadiliko makubwa katika mitizamo nimeona watu wakisema tuko upande wa Malala

Brown ambeye pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ameeleza alivyokutana na Malala na kile kilichomshangaza juu ya zawadi ya kuadhimisha kuzaliwa anayotaka mtoto huyo

(SAUTI BROWN)

Nilikutana na Malalaa alipokuwa hospitali alikpokuwa anapona kutoka katika majeruha,nimeona maendeleo makubwa aliyoyapta, alijeruhiwa sana na kukaa hsopitalini kwa meizi mingi na kufanyiwa upasuaji kadhaa na nimemuona akipata nafuu na hajawahi kupoteza nguvu katika maadili na unapomuuliza unataka nini katika siku hii ya kuzaliwa nasema anataka kujenga shule.