Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zisisahau kuchagiza sekta binafsi zinapoondoa vizuizi vya kibiashara: UNCTAD

Serikali zisisahau kuchagiza sekta binafsi zinapoondoa vizuizi vya kibiashara: UNCTAD

Serikali za Afrika zinafanya kampeni kubwa ya kupunguza vizuizi vya kibiashara baina ya nchi barani humo, lakini wakati zikifanya hivyo, zinapaswa zichukuwe hatua mathubuti kuzipa msukumo sekta za kibinafsi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Kamati ya Biashara na Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNCTAD, ambayo imeonya kuwa nchi za Afrika zisipotoa msukumo kwa sekta za kibinafsi, mfumo huu taratibu wa biashara utawafaidi wageni zaidi kuliko kampuni za kiafrika.Ripoti hiyo ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika 2013, imepewa kichwa: Biashara miongoni mwa Waafrika: Kufungua Uwezo wa Sekta ya Kibinafsi

Ripoti hiyo imekaribisha uamuzi wa viongozi wa Afrika wa Januari 2002 wa kuondoa vizuizi baina ya nchi zao ili kuupa msukumo biashara za kikanda. Hata hivyo, ripoti inasema biashara hiyo ya kikanda itatoa matumaini tu pale ambapo kampuni za Kiafrika zinazalisha bidhaa zinazouzwa.

Ripoti imeongeza kuwa ingawa kuondoa vizuizi ni muhimu, hakutazaa matunda yanayotarajiwa ikiwa hakutaambatana na juhudi za serikali kuoneza aina na ubora wa bidhaa ambazo zinazalishwa na chumi zao- yaani kupanua uwezo wa uzalishaji wao, wanavyosema wataalam wa kiuchumi.