Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya idadi ya watu duniani

Leo ni siku ya idadi ya watu duniani

Dunia ikiwa inaadhimisha siku ya idadi ya watu leo huku ujumbe wa maadhimisho hayo kwa mwaka huu ukiwa ni kutokomeza mimba za mapema , mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu UNFPA ndiyo wenye dhamana ya kuhakikisha ujumbe huo unawafikia walengwa na kutekelezwa kikamilifu.

Nchini Tanzania UNFPA kwa kushirikiana na wadau wanatoa elimu ya afya kwa vijana hususani wasichana juu ya madhara ya mimba za mapema.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami, Afisa wa UNFPA nchini humo Felista Bwana anasema ili kufanikisha swala hili mchango wa asasi za kiraia na serikali hauepukiki na hapa anaanza kufafanua kile kinachofanywa katika siku hii.

(SAUTI MAHOJIANO)