Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa waizuru kambi ya Ein El-Hilweh nchini Lebanon

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa waizuru kambi ya Ein El-Hilweh nchini Lebanon

Mratibu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Robert Watkins ameitembelea kambi ya Ein El-Hilweh iliyo kusini mwa Lebanon hii leo akiandamana na mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto kweye mizozo Bi Leila Zerrougui pamoja na mkurugezi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA nchini Lebanon Bi Ann Dismor.

Wote hao walishuhudia hali wanamoishi wakimbizi wa kipalestina na kuelezwa ugumu wa maisha miongoni mwa wakimbizi wa kipalestina waliotoka nchini Syria na jitida zinazofanywa na UNRWA kuwasidia. Wakati wa Ziara hiyo wakimbizi walielezea ugumu ya maisha wanaopitia nchini Lebanon, maisha yaliyo ghali na mihangaiko ya mizozo na vita. Walielezea matakwa yao ya kumalizika kwa mzozo nchini Syria ili waweze kurudi haraka makwao. Pia wote hao walielezwa kuhusu changamoto zinazolikumba Shirika la UNRWA haswa upande wa maji na chakula , miundo msingi kambini , afya na elimu. Hadi sasa kuna jumla ya wakimbi 71,000 wa kipalestina nchini Lebanon.