UM wakubali mwaliko wa Syria kukamilisha uchunguzi

11 Julai 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na profesa Åke Sellström, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa mataifa wa kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.Profesa Sellström amemweleza Ban hatua zilizofikiwa  ambazo ni pamoja na kuzichambua kwa kina taarifa walizopewa na nchi wanachama na shughuli za uchunguzinkatika nchi jirani.

Mwakilishi wa masuala ya upokonyaji silaha Bi Angela Kane, na profesa Sellström, wamekubali mwaliko wa serikali ya Syria kuzuru  Damascus kwa mtazamo wa kukamilisha kazi yao kwa misingi ya ushirikiano unaohitajika ili wawe huru, salama na waweze kukusanya taarifa za uchunguzi zinazotakiwa kuhusu madai ya matumizi ya silaha za kemikali kutumika katika taifa hilo la Kiarabu.