Tuwekeze kwa wasichana wabadili jamii: Ban

11 Julai 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezungumza katika siku ya idadi ya watu duniani na kusema ikiwa jamii itajitoa na kuwekeza raslimali za elimu ,afya na ustawi wa wasichana, kundi hilo litakuwa kichocheo kikuu kwa ajili ya mabadiliko chanya katika jamii.

Katika taarifa yake hiyo Ban amesema kuwa kufanya hivyo kutaleta mabadiliko kwa kizazi kijacho na kuongeza kuwa ni vyema kuwasaidia wasichana kutambua umuhimu wao ili wachangie katika mustakabali wa pamoja.

Akizungumzia maadhimisho ya siku hiyo, Afisa kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu UNFPA Felista  Bwana anazungumzia mikakati ya kuwanusuru vijana hususani wasichana kutumbukia katika mamba za mapema.

(SAUTI FELISTA)

Siku ya idadi ya watu duniani mwaka huu inaadhimishwa na ujumbe wa elimu dhidi ya mimba za mapema kwa lengo la kuwa na dunia yenye mimba zilizokusudiwa pekee.