Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nusu ya watoto wanaoacha shule wanaishi katika maeneo yaliyoathirika na migogoro:UNESCO

Nusu ya watoto wanaoacha shule wanaishi katika maeneo yaliyoathirika na migogoro:UNESCO

Waraka uliotolewa na utafiti wa kimataifa wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO unaonyesha kwamba nusu ya watoto milioni 57 ambao wameacha shule wanaishi katika nchi zilizoathirika na vita. Alice Kariuki anaripoti

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Ripoti hiyo iliyotolewa kwa ushirikiano na shirika la Save the children inaadhimisha miaka 16 ya siku ya kuzaliwa ya mtoto Malala Yousafzai ambayo ni Julai 12.

Malala ni binti wa Kipakistan aliyepigwa risasi na Taliban akiwa njiani kutoka shuleni Oktoba mwaka 2012. Waraka wake unaonyesha kwamba hatua za haraka zinahitajika ili kufikisha elimu kwa watoto milioni 28.5 wa umri wa kwenda shule za msingi ambao kwa sasa hawasomi katika nchi zenye vita. Tanzania hakuna vita lakini je hali ya elimu kwa watoto ikoje? Elizabeth Kyondo ni afisa wa UNESCO mjini Dar es salaam Tanzania.

(CLIP YA ELIZABETH KYONDO)

Kimataifa idadi ya watoto wasio mashuleni imepungua kutoka milioni 60 mwaka 2008 hadi milioni 57 mwaka 2011. Kwa mujibu wa UNESCO hata hivyo mafanikio hayo hayajafika kwenye nchi zilizoghubikwa na vita ambao kwa sasa wanafanya idadi ya asilimia 50 ya watoto ambao wanakosa elimu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8 kutoka asilimia 42 mwaka 2008.