Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Somalia walioko Kenya kurejeshwa makwao

Wakimbizi wa Somalia walioko Kenya kurejeshwa makwao

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa matifa la wakimbizi UNHCR Antonio Guterres yuko nchini Kenya ambapo pamoja na mambo mengine amefanya mazungumzo na maafisa wa serikali ya nchi hiyo kuhusu namna ya kuwezesha kuwarejesha makwao kwa hiari wakimbizi wa Somalia walioko Kenya kufuatia kile alichosema kuimarika kwa amani nchini Somalia.Yafuatayo ni mahojioano kati ya Msemaji wa UNHCR nchini Kenya Emanuel Nyabera na mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami kuhusu ziara ya Mkuu wa UNHCR Nchini Kenya.