Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gaye awasili CAR, kuongoza BINUCA

Gaye awasili CAR, kuongoza BINUCA

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kati Babacar Gaye amewaasili nchini humo tayari kuanza kazi hiyo akiwa ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Matifa wa kujenga amani nchini humo, BINUCA.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Bangui Bwana Gaye amethibitisha uteuzi uliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kuendeleza amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Amesema vipaumbele ni kuimarisha majadiliano ya kisiasa na kurejesha usalama katika ukanda huo pamoja na kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa na kutoa misaada ya kibinadamu.