Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marufuku ya matumizi ya virusi vya sotoka kwa ajili ya utafiti imeondolewa:FAO

Marufuku ya matumizi ya virusi vya sotoka kwa ajili ya utafiti imeondolewa:FAO

Marufuku iliyowekwa dhidi ya matumizi ya virusi hai vya sotoka kwa ajili ya utafiti imetolewa na shirika la chakula na kilimo FAO,kamainavyobaini ripoti iliyoandaliwa na Jason Nyakundi. 

(Taarifa zaidi na Jaison Nyakundi)

Amri hiyo ilitolewa kufuatia kutekelezwa kwa azimio mnamo tarehe mosi mwezi Mei mwaka 2011 na wanachama wa Shirika la linalohusika na afya ya mifugo lililowataka wanachama kutotumia  virusi vya ugonjwa sotoka bila ya idhini ya FAO na OIE.

Mashirika hayo mawili sasa yameweka mipangilio ya kufuata ili kuweza kupata idhini ya kafanya utafiti wowote  kwa kutumia virusi vya ugonjwa wa sotoka na bidhaa zilizo na virusi hivyo.

Kati ya mahitaji muhimu zaidi ni kuwa utafiti huo uwe na uwezo wa kuboresha usalama wa chakula  na kupunguza uwezekeno wa ugonjwa huo kujirurudia tena. Ugonjwa wa Sotoka ulitangazwa kuangamizwa mwaka 2011 lakini hifadhi ya virusi vya ugonjwa huo badi zipo kwenye mahabara.

Mwezi Juni mwaka 2012 amri ya kutumika kwa virusi hivyo iliwekwa baada ya FAO na OIE kugundua kuwa virusi hivyo vilikuwa  vikihifadhiwa kwenye zaidi ya mahabara 40 kote duniani.