Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila nchi ni lazima ichukue hatua za kupiga marufuku matangazo na ufadhili wa bidhaa za tumbaku:WHO

Kila nchi ni lazima ichukue hatua za kupiga marufuku matangazo na ufadhili wa bidhaa za tumbaku:WHO

Takriban mataifa 24 kote duniani yamepiga marufu matangazo ya bidhaa za tumbaku na ufadhili wake kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO. Flora nducha na taarifa kamili.

(PKG YA FLORA NDUCHA)

Kubuniwa kwa maneo yasiyo na moshi wa sigara ni moja ya hatua zilizochukuliwa na nchi 32 kwa kupiga marufuku uvutaji wa sigara maeneo ya umma, maeneo ya kazi na kwenye usafiri wa umma kwa muda wa miaka mitano iliyopita. Kwenye ripoti yake kuhusu janga la tumbaku Shirika la fya duniani WHO linasema kuwa zaidi ya watu bilini 3 wanalindwa na kampeni zinazopinga matumizi ya tumbaku maan kwamba mamilioni ya watu wasiovuta sigara wana uwezo mdogo wa kuanza kutumia tumbaku. Hata hivyo mataifa 67 bado yanaruhuus matangazo ya tumbaku na ufadhili mwingine. Mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Margaret Chan anasema kuwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na matumzi ya tumbaku vinatarajiwa kuongezeka hadi milonmi 8 ifikapo mwaka 2030.

Dr Douglas Bettcher ni mkurugezni katika kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza kwenye Shirika la WHO.

(SAUTI YA DR DOUGLAS BETTCHER)

”kuongezeka kwa masoko kuna maana kuongezeka kwa vifo, na sekta ya tumbaku ni mtambo wa kifo, na wanajisukuma zaidi na zaidi kweye nchi zinazoendelea kutafuta fursa penye matumizi ya tumbaku si ya juu miongoni mwa watu fulani. Ni muhimu kwa nchi zote kupiga marufuku aina zote na matangazo na ufadhili wa tumbaku. Hatuwezi kuruhusu sekta hii kuweka nembo zao kwenye fulana na kadhalika. Huwezi kuruhusu sekta hii kutoa zawadi za bure za tumbaku nje ya majumba ya densi na kadhalika. Ni lazima tupige marufuku haya yote kwa kuwa hii ndio njia ya pekee ya kuzima sekta ya tumbaku.”

Kulingana na WHO tumbaku ndiyo inaongoza kwa vifo vinavyoweza kuzuiwa ikiwa inasabaisha vifo milioni 6 kila mwaka duniani.