Mtaalamu wa UM kwenda Madagascar kuchunguza biashara ya ngono kwa watoto

10 Julai 2013

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Najat Maalla M’jid anatazamiwa kwenda nchini Madagascar kwa ajili ya kuendesha uchunguzi kuhusiana na ongezeko la biashara kuuza watoto na masuala ya kingono.Ziara hiyo imepangwa kuanza kufanyika Julai 15 hadi 26 mwaka huu.

Hii itakuwa ni ziara ya kwanza kwa mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya unyanyasaji watoto na utumikishwaji kwenye madanguron ya kingono.

Akizungumzia kuhusu ziara yake hiyo, mtaalamu huyo amesema kuwa watoto ndiyo waathirika wakumbwa wa matukio hayo yanayoripotiwa kutokea karibu duniani kote hivyo ametaka kuweka mazingira ya kujali ustawi wao

Kwenye ziara yake hiyo ambayo inakuja kufuatia ombi la serikali ya Madagasca, Bi Maalla anatazamia anatazamiwa kuwa na wigo mpana zaidi kuangazia hali jumla ilivyo pamoja na kujua chanzo cha kushamiri kwa biashara ya ngono na utumikishwaji wa watoto kwenye madanguro ya kingono.

Akiwa nchini humo mtaalamu huyo anatazamiwa kutembelea miji ya Antananarivo, Tulear, Nosy Be na Tamatave ambako atakutana na maafisa wa kiserikali ambao wapo kwenye vikosi kazi vya kukabiliana na biashara hiyo.

Ripoti itakayokusanywa na mtaalamu huyo inatazamiwa kuwasilishwa kwenye kikao cha baraza la haki za binadamu kinachotazamiwa kukutana Marchi 2014.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter