Mwakilishi wa UM awatakia Wasomali wote Ramadhan njema:Kay

9 Julai 2013

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Bwana Nicholas Kay, amewatakia Wasomali wote heri ya mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan.Wakati Wasomali wakiungana na Waislamu wote kote duniani kwa mfungo wa Ramadhan Kay amesema huu ni mwezi wa kiroho na kutafakari , na ni wakati mzuri wa kutimiza mambo mengi yanayohitaji kufanyika ili kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika kuelekea amani ya taifa hilo la pembe ya Afrika.

Amesema Somalia inahitaji kuendelea kupiga hatua ili kudumisha wajibu na ahadi zake kwa jumuiya ya kimataifa.

Kay ametoa wito kwa pande zote kujizuia na hatua zozote ambazo zitairudisha nyumba Somalia na kushindwa kufurahia uwezekano wa kuwa taifa huru la amani duniani. Na amewaambia Wasomali anawatakila kila la heri na mfungo wa Ramadhan wenye furaha na amani.