Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka Syria kumaliza machafuko wakati wa Ramadhan

Ban aitaka Syria kumaliza machafuko wakati wa Ramadhan

Wakati waisalamu kote duniani wakiwa wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelitaka taifa la Syria ambalo limekuwa katika mapigano kwa muda mrefu kuupatia suluhu ya kisaisa mzozo huo.

Akitoa wito wake kuhusu mfungo huo Ban amesema ni muhimu kuwafikia wahitaji wa vyakula , maji na dawa kwa majeruhi lakini akasisitiza kusimamisha mara moja kwa mapigano hususani kipindi hiki cha Ramadhani kwa kuzitaka pande zinzopigana kuheshimu mwezi huu ili uwe kama zawadi ya amani kwa watu wa Syria.

Katibu huyo Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anaamini suluhisho la mgogoro wa Syria itakuja kwa mazungumzo ya kumaanisha na kwmba Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia katika mchakato wa kusitisha mapigano kwa mustakabali wa kidemokrasia wa taifa hilo.