Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yanatishia usalama Misri: UM

Machafuko yanatishia usalama Misri: UM

Ofisi ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa umeelezea kusikitishwa kwake na kuendelea kwa machafuko nchini Misri kunakofuatia kuondolewa kwa serikali ya kundi la Muslim brotherhood.

George Njogopa anasimulia zaidi.

 Kiasi cha watu 90 wameuwawa tangu kuzuka kwa machafuko hayo ya kisiasa hapo July 3, huku idadi waliojeruhiwa ikifikia zaidi ya 1,3000.

 Kamishna wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa mamlaka zinapaswa kuanzisha uchunguzi wa wazi ili kuangalia mazingira ya mauwaji hayo ambayo yanazidi kuiweka katika hali tete Misri. Amesisitiza kuletwa kwenye mkono wa haki wahusika wa matukio hayo.

Lakini ametaka uchunguzi huo uendeshwe na chombo huru kisichofungamana na siasa za upande wowote na taarifa zake kuwekwa wazi kwa umma.

Kamishna huyo ameongeza kuwa mahali alipo kiongozi aliyepinduliwa Mohammed Morsi bado hakujulikani. Cécile Pouilly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI YA CECILE POUILLY)

“Tunatoa wito kwa pande zote zinazozozana kujiepusha na hali korofi na waandamanaji kuendesha shabaha ya kuwa na maandamano ya amani.Tumepata taarifa kuhusiana na mpango uliotangazwa na utawala wa mpito kuhusiana kuundwa kwa jopo ili kurekebisha katiba na kuwa na uchaguzi wa bunge.Tunatambua pia mpango huu umekataliwa na chama cha udugu wa kiislamu. Tunatoa wito kwa pande zote kujihusisha katika majadiliano yatayochukua maeneo yote ili kuiwezesha nchi kusonga mbele.’’