Ban ashutumu mauaji na ghasia zinazoendela Misri

9 Julai 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameelezea masikitiko yake kutokana  ghasia zinazoendelea nchini Misri wakati mzozo wa kisiasa unapoendela.Ban anasema kuwa anasumbiliwa na ripoti za kuuawa kwa zaidi ya watu 50 hii leo. Katibu mkuu ametuma rambi rambi zake kwa familia za wale waliouawa. Alice Kariki anaeleza zaidi.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Katibu mkuu Ban Ki moon amelaani mashambulizi hayo  akitaka kufanyika uchunguzi wa kina na mashirika yaliyo huru na wahusika kufikishwa mbele ya sheria. Ban ametoa wito kwa watu wote nchini Misri kukumbuka hali ilivyo nchini humo  na kufanya kila wawezalo kuzuia machafuko.

Kwa mara nyingine Ban amazitaka pande zote kujizuia akiongeza kuwa mandamano ni lazima yawe ya amani na vikosi vya usalama navyo ni lazima vizingatie sheria za kimataifa.

Ban pia ametaka Wamisri wote na vyama vya kisiasa kushirikiana na kuafikia uamuzi kwa njia ya amani. Ameongeza kuwa ili mpango huo uweze kufanikiwa  pande na jamii zote ni lazima zishirikishwe akisema kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kwa msaada wowote.