Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR azuru Moghadishu katika mkesha wa ramadhan na kuonyesha mshikamano:

Mkuu wa UNHCR azuru Moghadishu katika mkesha wa ramadhan na kuonyesha mshikamano:

Kamishina mkuu wa wakimbizi wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezuru Somalia Jumanne na kuonyesha uungaji mkono wake wa mchakato wa amani unaoendelea katika taifa hilo lililosambaratishwa na vita kwa zaidi ya miongo miwili.

Ziara yake ilipangwa ili kwenda sambamba na mkesha wa mfungo wa Ramadhan ili kuoshesha mshikamano wake kwa watu waSomaliakutokana na machungu ya kupita kiasi ynayowakabili.

Ndani yaSomaliainakadiriwa kuwa watu milioni 1.1 bado wametawanywa na kuzikihama nyumbao kutokana na vita, na wengine zaidi ya milioni moja wanaishu uhamishoni kama wakimbizi katika nchi jirani hususani,Kenya,EthiopianaYemenlakini pia idadi kuwa ya wakimbizi hao wakoDjibouti, bara Ulaya, Marekani naAustralia.

Guterres amesema huu ni wakati wa matumaini kwa watu waSomaliana UNHCR haiitaji zaidi ya kuwasaidia watu hawa kurejea makwao kwa hiyari yaona wakati ambao hali ni bora nna salama kufanya hivyo.

Ameongeza kuwa UNHCR inafanya kazi kwa karibu na serikali yaSomaliana nchi jirani zinazohifadhi wakimbizi wa Kisomali ili kujiandaa wakati uatakapowadia na amani ikiwa imerejea kwa watu hao kurejea nyumbani.

Wakati huohuo maelfu ya Wasomali wanaendelea kuikimbia nchi yao, katika miezi sita ya wanzo ya mwaka huu Wasomali 21,000 wamewasili katika nchi jirani kuomba hifadhi lakini vilevile wengine wanarejea nchini humo talkribani 20,000 wameingia Somalia huku 12,000 wakiwa ni wakimbizi halisi wanaorejea nyumbani.