Ban amemteua Aboulaye Bathil wa Senegal kuwa naibu mwakilishi Mali:

8 Julai 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza uteuzi wa Adulate Bathily wa Senegal kuwa naibu mwakilishi wake maalumu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Mali MINUSMA.Bwana Bathily amekuwa akifanya kazi kama waziri katika ofisi ya Rais nchiniSenegaltangu mwaka 2012.

 Mwaka 1998 hadi 2001 alikuwa mbunge  kabla ya kushika wadhifa wa naibu spika kati ya mwaka 2001 hadi 2006. Amejiuhusisha na jumuiya mbalimbali ikiwemo ECOWAS, Muungano wa Afrika wakati wa machafuko yaMadagascarna kusuluhisha migogoro mbalimbali ya Afrika ya Magharibi ikiwemoLiberia,Sierra Leone, Guinea Bissau, Niger,GuineanaMali.

 Bwana Bathily ana stashahada ya udaktari yaani PhD ya masuala ya historia kutoka chuo kikuu cha Birmingham nchini Uingereza . Alizaliwa cnhini Senegal mwaka 1947 na ni baba wa watoto wanne.