Ban atuma rambi rambi zake kutokana na ajali ya ndege iliyotokea jimbo la Carlifonia nchini Marekani

8 Julai 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameelezea huzuni yake baada ya ajali ya ndege ya shirika la Asiana iliyotokea kwenye eneo la San Fracisco jimbo la California nchini Marekani mwishoni mwa juma.Ban ametuma rambi rambi zake kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao za wale waliojeruhiwa na wengine walioathiriwa na ajali hiyo kwa njia moja au nyingine.

Ban pia ameonyesha huruma zale kwa serikali na watu  wa China nyumbani kwa wengi wa wahanga wa ajali hiyo. Katibu mkuu pia amepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na utawala wa Marekani katika kupunguza maafa zaidi.