Mashindano ya 24 ya Tennis ya vijana kufanyika kwa msaada wa UNESCO

8 Julai 2013

Mashindano ya 24 ya vijana ya mchezo wa tennis , yajulikanayo kama BNP-Baribas Cup safari hii yanafanyika chini ya mwamvuli wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.Mashandinando hayo yatawaleta pamoja wachezaji kutoka kila pembe ya dunia kuanzia leo tarehe 8 Julai hadi tarehe 14 Juali mwaka huu karibu na mji waParisnchini Ufaransakamainavyoaribu taarifa ya Jason Nyakundi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kwa juma zima vijana hawa watashindana chini  ya wafadhili watatu katika awamu ya mwaka 2013.Kama ilivyo mechi hizo za vijana za mpira wa tenisi za OPEN stade Francais zitakuwa na mafunzo  na zitakuwa zenye kauli mbiu kuhusu maendeleo endelevu na ulemavu.

Washiriki ambao ni vijana watakuwa na fursa ya kushirikia kwenye shughuli nyingi  nje ya uwanja ambapo mikutano ya kupinga matumizi ya madawa ya kusisimua misuli na hatari zake itaandaliwa.

Maonyesha , warsha za elimu, michezo kuhusu uendeshaji baiskeli vyote vitakuwepo. Wakati wa mechi hizo zawadi itatolewa kwa kijana ambaye ataonyesha nidhamu ndani mwa uwanja na nje.

Kupitia kwa waandalizi mkurugenzi mkuu wa Shirika la elimu , Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amesema kuwa kwa zaidi ya mwongo mmoja UNESCO imekuwa ikiunga mkono micchezo elimu na utamaduni.