Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama inatia shaka Sudan: UM

Hali ya usalama inatia shaka Sudan: UM

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba mapigano nchiniSudankati ya majeshi ya serikali na waasi yaliyosababisha vifo vya wafanyakazi wawili wa asasi za kiraia huko Darfur ni  ishara ya kudorora kwa usalama na kikwazo cha kufikisha misaada katika jimbohilolenye mizozo.

(TAARIFA YA GEORGE)

Mratibu wa shughuli za misaada ya kibinadamu nchini Sudan Ali Al-Za'tari,amelaani mauwaji hayo kwa kusema kuwa wafanyakazi hao wako Darfur kwa ajili ya kusaidia misaada ya kiutu hivyo kitendo cha kuwashambulia na kufifisha maisha yao hakikubaliki.

 Bwana  Al-Za'tari amesema kuwa Umoja wa Mataifa umeingiwa na simanzi  kutokana na kupoteza kwa watumishi wake waliokuwa wakifanya kazi na shirika la kimataifa la World Vision linaendesha shughuli za usamaria mwema.

Mapigano hayo baina ya vikosi vya serikali na makundi ya wanamgambo yamesababisha kujitokeza kwa hali ya sintofahamu.

Mfanyakazi mwingine wa shirikahiloameripotiwa kuwa katika hali mbaya na amekimbizwa hospitali kwa matatibabu.

Kauli ya kutaka kuwepo utulivu kwenye eneohiloiliyotolewa na Bwana Al-Za'tari inafuatia kauli nyingine kama hiyo iliyotolewa Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu juu ya vikosi vya ulinzi wa amani Hervé Ladsous ambaye alitaka pande zinazozozana kuweka chini silaha.