Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yalaani mauaji ya watoto Nigeria

UNICEF yalaani mauaji ya watoto Nigeria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limelaani mauaji ya watoto nchini Nigeria ambapo trakwimu zinaonyesha kwamba tangu June 16 mwaka huu idadi ya watoto 48 na walimu 7 wameuwawa katika mashambulizi manne yaliyoripotiwa katika jimbo la Kaskazini.

Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Magharibi na Kati mwa Afrika Manuel Fontaine pamoja na kutoa rambirambi kwa wahanga wa matukio hayo, amesema hakuna namna yoyote ya kuhalalisha maujai hayo na kutoa wito wa kufikishwa katika vyombo vya sheria watendaji wa vitendo hivyo ili jamii itazame shule kama sehemu ya amani.