Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mustakabali wa lugha ya Kiswahili unaridhisha:Mwinyi

Mustakabali wa lugha ya Kiswahili unaridhisha:Mwinyi

Wiki chache baada ya ripoti ya maendeleo ya binadamu ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP kuzindiliwa kwa Kiswahili, Rais mstaafu wa Tanzania Al Hasani Mwinyi amesema lugha hiyo sasa inakuwa kimataifa na kutaka vyombo vya habari kuisambaza maradufu.

Taarifa zaidi na Grece Kaneiya

Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa tamasha la utamaduni wa Kiswahili mjini Washington DC Rais huyo mstaafu wa Tanzania amabaye amekuwa akipigia chapuo lugha hiyo amesema anafarijika kuona taasisi za kimataifa zinakitumia Kiswahili kama nyenzo ya mawasiliano.

(SAUTI MWINYI)

Kwa Upande wake Mhadhiri mwandamizi wa lugha ya Kiswahili katika chuo kikuu cha Indiana Profesa Deo Tungaraza anaelezea namna chuo hicho kinavyofundisha lugha hiyo kwa mbinu mbadala ili kufikia ulimwengu.

(SAUTI PROF DEO)