Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ladsous , Chambas wafanya ziara Sudan

Ladsous , Chambas wafanya ziara Sudan

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika opersheni za kulinda amani Hervé Ladsous akiambatana na mwakilishi wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika operesheni huko Darfur (UNAMID) Muhamed Ibn Chambas wametembela Sudan.

Katika ziara hiyo iliyoanza July 3, Ladsous alikwenda El Daein huko katika jimbo la Darfur Mashariki ambapo alikutana gavana na viongozi wengine wa kijamii katika eneo hilo wakiwamo wa asasi za kiraia kadhalika wakimbizi wa ndani katika kambii iitwayo Neem.

Msaidizi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia alikutana na rais wa Sudan Omar Ali- Bashir na maafisa waandamizi wa serikali ya Sudan.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Khartoum Ladsous ameelezea kusikitishwa kwake na mgogoro unaoendela katika jimbo la Darfur ambao unaathiri idadi kubwa ya raia na kuongeza kuwa hali ya usalama imeendelea kuzorota.