Bado watu wasalia kambini miaka mitatu unusu baada ya tetemeo la ardhi nchini Haiti:IOM

5 Julai 2013

Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM limetoa ripoti yake kuhusu kuhama kwa watu nchiniHaiti  ikiwa ni miaka mitatu unusu tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu mkuwa  kwenye kisiwa hicho mwaka 2010.Ripoti hiyo inaonyesha kwa watu 279,000 wakimbizi wa ndani ambazo ni familia 71,000 bado wako kwenye kambi za wakimbizi wa ndani  na maeneo mengine nchini humo.

Tangu kutokea kwa jangahilo  kumeshuhudiwa kupungua kwa asilimia 82 ya watu waliohama makwao na kupungua kwa kambi za wakimbizi wa ndani kwa asilimia 77. Ripoti hiyo inaangazia robo ya pili ya mwaka 2013 kati ya mwezi Aprili na Juni ikionyeshea kupungua kwa kiasi kikubwa cha wakimbizi  wa ndani tangu mwezi Aprili mwaka 2012.

Maeneo 33 yalifungwa huku watu 41,000 wakihamishiwa kwingine. Jumbe Omari Jumbe anafafanua zaidi

(CLIP YA JUMBE OMARI JUMBE)