Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia walindwe Misri : Pillay

Raia walindwe Misri : Pillay

Siku mbili baada ya jeshi nichini Misri kutangaza kumwondoa madarakani rais wa Misri Muhammed Morsi, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Matifa Navi Pillay amezitaka pande zote nchini humo kuhakikisha haki za raia zinaheshimiwa na kulindwa wakati hali ya sintofahamu ikiwa imetanda katika taifa hilo lililoko kaskazini mwa Afrika

George Njogopa na taarifa kamili

(SAUTI YA GEORGE)

Pillay amesema kuwa binafsi anawaunga mkono raia wa Misri wanapigania na kutetea utaifa wao kwa shabaha ya kulinda haki zao za msingi na uhuru wa maoni ambao ulidaiwa kubinywa wakati wa utawala wa Mohamed Mosri aliyeondolewa madarakani kwa shinikizo la wananchi na kuungwa mkono na jeshi.

Amesema kuwa maandamanao makubwa yaliyokuwa yakishuhudiw katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita, ulikuwa ujumbe tosha kwamba wananchi wa Misri walikuwa wakipigania kile alichokiita kuheshimiwa kwa haki zao za msingi.

Kwa upande mwingine amesema kuwa anatumai serikali mpya iliyoko madarakani ambayo ni ya mpito itaanzisha juhudi za kurejesha utawala wa kisheria na kutoa haki kwa raia wote wa Misri.

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu