Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na GRETA waungana kupambana na usafirishaji haramu wa watu Ulaya na kwingineko

UM na GRETA waungana kupambana na usafirishaji haramu wa watu Ulaya na kwingineko

Wataalamu wa mashirika mawili muhimu ya kimataifa yanayopambana na usafirishaji haramu wa watu wameungana kuimarisha uwezo wa kukabiliana usafirishaji haramu wa watu barani Ulaya na kwingineko.Karibu watu milioni 21 ni wahanga wa kazi za shuruti na usafirishaji haramu wa watu duniani wakiwemo takribani watu milioni moja kwenye muungano wa Ulaya.

Takwimu hizi ni kwa mujibu wa wa shirika la kazi duniani ILO. Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu usafirishaji haramu wa watu hususani wanawake na watoto Joy Ngozi Ezelio na baraza la Ulaya la kundi la wataalamu kuhusu hatua dhidi ya usafirishaji haramu wa watu GRETA wameimarisha msimamo wao kwenye mkutano wa kwanza kabisa wa kujadili njia mpya, hatua za pamoja na kuimarisha ubadilishanaji wa taarifa kutu tatizo la usafirishji haramu wa watu.

Wataalamu 15 wa GRETA wenye uzoefu na utaalamu watasaidia kuja na mtazamo madhubuti wa kupambana na tatizo hili sugu barani Ulaya na kwingineo amesema Bi Ezeilo.

Kauli hiyo ya Bi Ezeilo imekuja wakati wa mkutano maalumu ulioandaliwa na GRETA huko Stausbourg Ufaransa kujadili masuala muhimu yanayohusiana na ngazi ya kitaoifa ya kutafsiri suala la usafirishaji haramu wa watu na makundi maalumu yaliyoko katika hatari ya kusafirishwakamawatoto.

Pia wataalamu hao wamebadilishana mawazo ili kuboresha ushirikiano wa kazi baina ya GRETA na Umoja wa Mataifa.