Hali CAR bado ni tete, vigumu kuwafikia raia walio na hofu kubwa:UNHCR

5 Julai 2013

Miezi mitatu baada ya kuondolewa madarakani serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa hofu na hali ya wakimbizi wa ndani takribani 200,000 na wakimbizi wengine zaidi ya 20,000.Mwezi mmoja uliopita UNHCR pamoja na washirika wao wamekuwa na fursa ndogo saana ya maeneo ya Bangui pamoja na vitongoji vingine vya ndanindani mwa nchi hiyi kama Ouham, Batangafo, Bambari, Kaga Bandoro na Mbaiki.

Ziara yaom aeneo hayo ilikuwa ni ya kutathimini hali halisi ya watu walioathirika na machafuko ya karibuni na matokeo ya tathimini hiyo kwa mujibu wa UNHCR inatia mashaka.

Kwa ujumla UNHCR inasema bado ni tete kwa ukosefu wa usalama na kutofuata sheria kumetapakaa. Wafanyakazi wa UNHCR wamepokea taarifa kwamba watu wanakamatwa hovyo , wanazuiliwa kinyume cha sheria , wanateswa, kuawa, ujambazi wa silaha unafanyika, mateso ikiwemo ukatili wa kimapenzi, ubakaji, kujaribu kubaka, utekaji, kuzuiliwa kutembea, uporaji  na mashambulizi dhidi ya raia. Pia makundi ya watu wenye silaha wamechoma vijiji na nyumba katika baadhi ya maeneo.

Kwa mujibu wa UNHCR ukatili dhidi ya wanawake, wasichana na wavulana umeongezeka.Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamekuwa yakitoa msaada na ushauri nasaha kwa waathirika katika baadhi ya maeneo.