Nafuatilia yanayoendelea Misri:Ban

4 Julai 2013

Katibu Mkuu wa Umoha wa Mataifa Ban Ki-moon anafuatilia kwa karibu maendeleo ya haraka yanayotokea Misri kwa makini na hiofu. Amesem   hata hivyo anasiamama na matakwa ya watu wa taifahilo.

 Kipindi cha mpito nchini Misri chajikuta njia panda tena kufuatia hatua ya keshi kutangaza kwamba inasitisha katiba na kumteua mkuu wa mahakama ya katiba kuwa Rais wa mpito, uamuzi ambao haujakubaliwa na Rais Morsy.

Katika kipindi hiki cha kuendelea kuwa na mvutano na hali ya sintofahamu nchini humo Katibu Mkuu Ban amerejea kutoa wito wa kuwa na utulivu, kuacha machafuko, kufanya majadiliano na kujizuia na ghasia.

Amesema mtazamo unaojumuisha pande zote ni muhimu saana katika kushughulikia haja na matatizo ya raia wa Misri. Utekelezaji wa haki za msingi ikiwemo uhuru wa kuongea na kukusanyika ni muhimu saana ameongeza Ban.

Katika maandamanoyaoWamisri wengi wameelezea mattizo kibao. Wakati huohuo uingiliaji wa jeshi katika masuala ya taifa inatia hofu. Hivyo amesema Ban iotakuwa muhimu kurejeshwa haraka utawala wa kiraia  kwa kuzingatia misingi ya kidemokrasia.

Mwisho Ban amewakumbusha Wamisri kuwa dunia inaangali ni hatua gain itakayofuata, akitumai kwamba Wamisri watasalia kuwa na amani, wakishinda magumu wanayoyapitia sasa na kutafuta muafaka wa pamoja ili kusonga mbele na kipindi cha mpito suala ambalo wananchi wengi wamelipigania kwa matumaini makubwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter