Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watunga sera watambue mchango wa wakulima: FAO

Watunga sera watambue mchango wa wakulima: FAO

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la  chakula na kilimo duniani FAO inasema watunga sera wanatakiwa kutambua michango tofauti ya wakulima wadogowadogo wanapowaunganisha na masoko ili kuwawezesha kulisha watu wengi zaidi.Alice Kariuki unafafanua zaidi(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Ripoti hiyo imesisitiza haja ya kuwa na ushirikiano wa kibiashara kwa ajili ya kupanua soko na kuongeza ubunifu wa utumiaji wa teknolojia  ya kisasa ili kufikia shabaha ya kuwa na uzalishaji imara.

Lakini kwa upande mwingine,FAO katika ripoti yake hiyo imezungumzia haja ya kubuniwa kwa sera zitazowatambua wazalishaji wadogo wadogo.

Aidha ripoti hiyo imesema kuwa kuwawezesha wazalishaji wadogo wadogo kunaweza kupanua uwigo wa mauzo hatua ambayo inaweza kutoa faida kubwa kwa familia nyingi.

Kwa upande mwingine ripoti hiyo imetaja eneo linalopaswa kuzingatiwa ikiwemo lile la kuwa na mwingiliano wa karibu baina ya wakulima na wanunuzi kwani kwa kufanya hivyo kunasaidia kuongeza tija.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa kwa kufanya hivyo kutatoa unafuu kwa wakulima wengi kutotumia muda wao kwenye safari.