Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa AU akutana na rais wa Somalia pamoja na waziri mkuu

Mjumbe wa AU akutana na rais wa Somalia pamoja na waziri mkuu

Mjumbe maalum wa Muungano wa nchi Afrika nchini Somalia balozi mahamat Saleh Annadif hii leo amemtembelea rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahamud pamoja na waziri mkuu wa nchi hiyo Abdi Farah Shirdoon.Wote hao walizungumzia masuala kadha zikiwemo ghasia zilizoshuhudiwa hivi majuzi mjini kismayo. Mjumbe huyo pamoja na rais walijadili njia za kumaliza taabu za watu kwenye mji wa Kismayo kwa kushirikina na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM.

Balozi Annadif amerejelea kauli yake ya kujitolea kwa AMISOM kwa manufaa ya watu waSomalia akisisitiza kuwa suala la kuhakikisha kuwa watu wa Somlia wanaishi kwa usalama ndiyo ajenda kuu ya AMISOM.

Amesema kuwa AMISOM imeyatilia maanani majukumu yake na itaendelea kushirikiana na na serikali ya Somalia na vikosi vyake vya usalama katika kuleta utulivu nchini humo.